Monday, April 10, 2017

Rais Magufuli ateua kamati ya pili itakayofanya uchunguzi wa kiasi cha madini yaliyopo kwenye mchanga uliopo maeneo mbalimbali nchini

Rais Magufuli ateua kamati ya pili itakayofanya uchunguzi wa kiasi cha madini yaliyopo kwenye mchanga uliopo maeneo mbalimbali nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Aprili, 2017 ameteua wajumbe wa kamati maalum ya pili itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kamati hiyo inajumuisha wachumi na wanasheria na imetanguliwa na kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni;

    Prof. Nehemiah Eliachim Osoro    Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara    Dkt. Oswald Joseph Mashindano    Bw. Gabriel Pascal Malata    Bw. Casmir Sumba Kyuki    Bi. Butamo Kasuka Philip    Bw. Usaje Benard Usubisye    Bw. Andrew Wilson Massawe

Wajumbe hao wataapishwa na Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

10 Aprili, 2017

No comments:

Post a Comment